TATIZO LA UUME KUSINYAA WAKATI WA TENDO


TATIZO LA UUME KUSINYAA

Mwanaume anayepatwa na tatizo hili anapokuja kujigundua huona kama mabadiliko makubwa yaliyotokea ghafla katika viungo vyake vya siri. Mwanamke mwenye tatizo hili pia naye huona kama tatizo geni linaloanza ghafla. 

Kwa kawaida hali hii hutokea katika umri mkubwa kwa mwanaume na mwanamke yaani kuanzia umri wa miaka hamsini lakini ikitokea katika umri chini ya miaka hamsini basi ni tatizo. Wapo vijana wenye matatizo haya ambayo vyanzo vyake tutakuja kuviona katika safu hii.

CHANZO CHA TATIZO

Hali ya kusinyaa kwa viungo vya uzazi kwa mwanamke na mwanaume hutokana na kuwepo kwa msukumo hafifu wa damu sehemu hiyo, maambukizi sehemu za siri ambayo huwa ya muda mrefu hasa kaswende, hitilafu katika misuli ya uke na sehemu za siri za mwanaume inayoathiriwa na kaswende virusi vya HIV, ugonjwa wa kifua kikuu na hata baadhi ya magonjwa sugu ya ngozi. Matatizo mengine yanayochangia hali hii ni ugonjwa wa kisukari.


Matatizo katika mishipa ya damu vilevile huweza kusababishwa na magonjwa ya moyo au mishipa ya damu inayosambaa sehemu hizo. Misuli inaposinyaa kwa mwanamke nayo huweza kusababishwa na magonjwa kama tulivyoona, uke unasinyaa pia huweza kusababishwa na uzazi wa mara kwa mara na karibu kufanya ngono mara kwa mara na wanaume tofauti na hitilafu katika mfumo wa homoni. 



Mwanamke anapata tatizo hili la kusinyaa uke endapo pia homoni au kichocheo cha Estrogen' kitakuwa kimepungua mwilini na kufanya mafuta yapungue ukeni. Kwa upande wa mwanaume homoni inayopungua kwa mwanaume ni Testosterone.



DALILI ZA TATIZO
Mwanaume mwenye tatizo hili hasa kijana, ingawa kwa wazee ni hali ya kawaida, kijana huanza kuona mfuko wa pumbu hulegea na kushuka sana, usinyaa na kujikunja kunja, kokwa huinekana ndogo na mishipa mikubwa ya damu huanza kujitokeza na mishipa mbegu toka katika kende huonekana wazi. Uume huwa kama wa mtoto mdogo na mishipa ya damu huchomoza wazi. Nguvu za kiume hupungua sana na endapo ukiweza tendo la ndoa la kwanza unawahi kumaliza na kushindwa kabisa kupata tendo la pili.



Mara kwa mara maandalizi kabla ya tendo la ndoa kwa mwanaume mwenye tatizo hili ni kuchezea sana uume kwa kuurusharusha au kuupiga piga kidogo kidogo ili kuamsha au kuhamasisha msukumo wa damu. Baada ya hapo uume huanza kusimama taratibu na endapo utasimama basi inabidi uwahi tendo na kama utachelewa, basi uume utalala na kushindwa tena kufanya tendo kwa siku hiyo. 



Mwanamke yeye daima huwa mkavu na wakati wa tendo hapati hisia zozote hadi tendo linapokwisha na kama mwanaume hana tatizo lolote na mwenye nguvu za kutosha basi mwanamke atapata michubuko na maumivu na kuhisi karaha ya tendo na hawezi kufika kileleni.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »